KUHUSU WANYOFU


Jumuia ya Wanyofu ni jamii ya watu kutoka dini zote inayohubiri Matendo Mema, Mamlaka ya Nafsi pamoja na Ukweli kuhusu mwanadamu na ulimwengu unaomzunguka.

pia Unyofu ni dini inayojitegemea yenye kujiegemeza si katika maandiko fulani matakatifu bali yenye kujiegemeza katika ukweli kama ulivyofunuliwa kwa binadamu kupitia ufahamu na uthibitisho, kisaikolojia, kisayansi na kiroho.

Kwa hiyo kama mtu anayejiunga, anataka kuwa mwana jumuia pekee kutokea dini nyingine na akaendelea na dini yake anaruhusiwa asilimia zote. kwani Unyofu unaheshimu dini zote. (lakini tu hautafumbia macho itikadi yoyote mbovu inayozidi kuiweka jamii ya binadamu katika usingizi kiroho).
Kama mtu aamua mwenyewe kuwa hii ndio dini yake moja kwa moja pia anaruhusiwa asilimia zote.
Kwa hiyo ni ruksa, vyo vyote vile ukweli utaenea--Tunataka tujenge timu imara yenye kubeba dhamana ya dunia hii.
   
(Bofya Hapa Kusoma  KWA NINI TUNAITWA WANYOFU?)

Jumuiya hii sio ya siri bali inaweza kukuwekea mezani siri nyingi ambazo zimefichwa kwa karne nyingi hata zile siri zilizo katika jamii za siri. Kwa lengo tu la kufungua macho yako ili kuondokana na utumwa wa kifikra na kiroho. Siri zozote ambazo huzijui na zinaweza kufumbua macho yako zinawezekana kupatikana katika jumuiya hii. Ni hiyari yako kuzikubali au kuzikataa na pia ni hiyari yako kufanyia utafiti wako binafsi.

Jumuiya hii haifungamani na upande wowote bali inafungamana na ukweli wowote uliothibitka kiakili, kisayansi na hata kiroho. Jumuiya haisiti kuachilia itikadi yoyote iliyonayo endapo itathibitika kwa vigezo sahihi kua itikadi hiyo siyo ukweli ni upotofu. Na ndio sababu nguzo za Jumuiya hii zinaweza kuongezeka au kubadilika wakati wowote kadiri ukweli unavyofunuliwa katika jamii ya binadamu na ulimwenguni kote.

Jumuiya haina madai yoyote kua yenyewe peke yake ndio ina ukweli kamili eti kwaajili ya vizazi vyote. (Bofya hapa kusoma UNYOOFU UNAAMINI NINI?)

Jumuiya haina muungano wowote  na jamii yoyote kati ya zile ziitwazo jamii za siri kama vile jamii ya Wa- essenes iliyoanza takribani miaka ya 100 kabla ya Yesu, na nyinginezo nyingi za kisasa, na wala haiwazuii wanachama wa jumuiya hizo kua wanachama wa jumuiya hii ya wanyofu.

Moja kati ya mafundisho makuu ya Wanyofu:-

Ukombozi wa kweli kupitia maarifa

Hii ni moja kati ya mafundisho makuu ya Wanyofu:-
Changamoto pekee inayomkabili binadamu ni matumizi makamilifu ya maarifa. Hakuna changamoto kuu kuzidi uwezo wa binadamu. Changamoto zote zinazomkabili binadamu ni kwa sababu hajui maarifa ya kuondoa changamoto hizo. Kimsingi watu hawaangamii kwa sababu ya majaribu au matatizo, watu huangamia kwa sababu ya ukosefu wa maarifa. Maana hakuna jaribu linalowazidi binadamu, majaribu yote duniani ni matokeo ya kiwango kidogo cha maarifa kilichopo hadi sasa. Kwa kadiri maarifa yanavyozidi kuongezeka na changamoto husika zinaondoka. Jawabu kwa kila tatizo ni maarifa.
Wanyofu hatungojei msaada kutoka nje ya sayari dunia, kwa sababu huo sio mtindo husika wa matumizi ya Mamlaka ya Nafsi. Mamlaka ya Nafsi ya binadamu ndiyo yenye jukumu la kuondoa matatizo yote ya binadamu, kwa sababu Mungu alituumba na viwekezo vyote vinavyohitajika ili kutawala dunia na kuitiisha. Ndiyo maana changamoto zote zinazomkabili binadamu zimo ndani ya uwezo wake, kupitia matumizi sahihi ya maarifa. Hatuhitaji kutafuta msaada nje yetu, kwa kila tatizo jawabu lake limo ndani yetu. Na hakuna tatizo lisilo na jawabu, kwa sababu kwa mujibu wa kanuni inayotawala ulimwengu, kanuni ya jozi, kila hasi kuna chanya, kila kushoto kuna kulia, mashariki kuna magharibi,kusini kuna Kaskazini, baridi kuna joto, giza kuna nuru. Kwa hiyo kama kuna tatizo basi kuna jawabu. Hii ndiyo inaruhusu binadamu kutumia uwezo wake wa kuchagua. Maana ili uweze kuwa huru kuchagua sharti ziwepo pande mbili tofauti na tena kuwe na uwezo kamili wa kuchagua upande mmojawapo. Binadamu ana uwezo wa kuchagua ama maisha yasiyo na matatizo au maisha ya matatizo yasiyokoma kwa kukuza viwango vya maarifa, upendo na heshima au kutojishughulisha kuvikuza kabisa.

 (Also Biological problems like sicknesses and diseases, old age or even death shall be also solved during the perfect knowledge day known as perfection day. Wanyofu, we do believe that all things are possible).
(BOFYA HAPA kusoma KUHUSU UWEZO USIO NA MIPAKA WA BINADAMU)

MUNGU NI ROHO

Sisi Wanyofu tunaamini kwamba Mungu ni Roho. Roho maana yake ni nini? Miongoni mwa Walimu tunaowaheshimu ni Bwana Yesu. Yesu ndiye aliyeleta wazo hili kwamba Mungu ni Roho. Alifafanua maana ya neno roho hapo alipowaambia wanafunzi wake kwamba roho haina mwili wala mifupa. Kutokana na maana yake hiyo ya neno roho, kumbe roho ni kitu kisicho na mwili wala mifupa. Kwa hiyo Mungu hana mwili wala mifupa. Miongoni mwa vitu visivyo na mwili hapa duniani ni kama nguvu, maji na hewa. Je hiyo yaweza kuwa ndiyo namna ya umbo la Mungu? Mfalme Sulemani anatusaidia zaidi anaposema kwamba Mungu mbingu hazimtoshi. Je anaweza kuwa amezijaza mbingu mithili ya hewa? Dhana hii hukaziwa tena na tena na baadhi ya walimu wa kale wa kiebrania, kwa mfano Mfalme Daudi anasema niende wapi nijiepushe na Roho yako, nikishuka kuzimuni upo, ningepanda mbinguni upo, ningeenda baharini huko nako utaniongoza. Yeremia anaripoti kwamba mbingu na dunia zimejawa naye. Kwa hiyo kwa mujibu wa walimu hao wa kale, Mungu hana umbo maalumu, na ndiyo maana anaweza kujaza mbingu na zisimtoshe, kama angekuwa na umbo maalumu, umbo hilo lingeweza kuizuia asijaze mbingu. Pia dhana kwamba Mungu hana mwili ndiyo dhana sahihi kwa yule aliyeasisi ulimwengu, maana kama angekuwa na umbo pamoja mwili kungezua maswali kwamba nani aliyeviumba? Aidha ni kwa nini haonekani ni kwa sababu ni Roho. Pia ni kweli nini hana sanamu ni kwa sababu hiyo hiyo, yeye ni Roho, hana umbo.
Wataalamu wa theolojia wanasema kwamba Mungu ni Omnipresent, yaani yupo kila mahali, kauli hii inathibitisha kile Wanyofu tunaamini kwamba Mungu hana umbo ,ni kama maji au hewa.
Kwa maana hiyo sisi Wanyofu tunaamini kwamba Mungu yupo kila mahali, na kwamba hana kulia kwake wala kushoto kwake kwa sababu ameenea pote. Nafasi yoyote hata kama ni ndogo namna gani Mungu yupo hapo.
Kwa sababu hiyo sisi Wanyofu tunaamini kwamba Mungu anaishi angani, kama tu walimu wa kale waliofundisha kwamba Mungu anaishi mbinguni, na jina mbingu maana yake ni anga kwa sababu kitabu cha Mwanzo chasema, Mungu akaliita anga mbingu. Ni kama pia tu Nabii Isaya alivyoandika kwamba mbingu (anga) ndicho kiti cha Enzi cha Mungu. Mungu wa milele hangehitaji kiti cha kutengenezwa ili aweze kukaa, maana kabla ya hicho kiti kuumbwa alikuwa hana pa kukaa? Ni kama pia hana sayari maalumu anapoishi maana sayari pia ni kiumbe chake, tuseme kwamba aliishije kabla ya kuumbwa kwa sayari hiyo, vinginevyo sayari nayo ingepaswa kuwa ya milele kama Mungu.
Mungu hana umbo maana ni Roho tupu. Bwana Yesu aliposema kwamba Mungu ni Roho alisema pia tunapaswa kumuabudu katika roho, ndio kusema na sisi tunazo roho. Sisi Wanyofu tunaamini kwamba roho zetu ni sehemu ya pili na ya tatu ya ufahamu unaojulikana kama Sub conscious mind na Super conscious mind. Sehemu hizi ni za kimungu katika asili yake, ni uungu ndani yetu. Ni sehemu ya Mungu mwenyewe ndani yetu. Ndiyo maana Bwana Yesu hapa na pale alisema kwamba Mungu yumo ndani yake.
Mungu ni Roho kwa hiyo hana mwili wala jinsia. Kwa sababu hiyo tunaamini kwamba Mungu siyo baba wala mama, kwa sababu roho haina mwili wa jinsia. Mungu sio jinsia ya kiume wala ya kike. Na pia sababu ya nguzo ya pili ya Unyofu yaani Kanuni za Asili, kila umbile lina kazi yake wala hakuna umbo la bahati mbaya. Hivyo tungepaswa kujiuliza, kwamba Mungu anakuwa wa kiume au wa kike ni ili afanye nini? Kwa hiyo Mungu ni Roho tupu, hana mwili, umbo wala jinsia. Yeye ni Roho, na kwa hiyo tunaposema Roho ya Mungu ni kusema sehemu ya Mungu, kwa maana Mungu ni Roho.
Pia kwa sababu ya uwepo wa Mungu wa mahali pote , sisi tunamfahamu Mungu anayepatikana pote, na wakati wote. Hana mji, sehemu au wakati anaopatikana zaidi ya mwingine. Nyakati zote, mahali popote anapatikana. Kwa hiyo kigezo chetu katika kumuabudu siyo mahali wala wakati bali ni hali zetu za kiroho na mazingira au Nyakati zinazoruhusu hali hizo. Kwa hiyo suala siyo upande wa Mungu bali upande wetu.
Mungu hapatikani kwenye sayari fulani huko mbinguni, ni Mungu yule aliyepo mbinguni aliyepo duniani,aliyepo mahali pote.
Kwa sababu ya umbo hili la Mungu, hahitaji kuumbwa ili awepo, kwa sababu Roho haina mwanzo wala mwisho. Na ndiye chanzo cha nguvu zote. Kuna Msemo mmoja wa kisayansi unaosema kwamba "Energy can neither created nor destroyed but can be transformed from one energy to another" Kwa hiyo Mungu kwa sababu ya asili hii ya uungu, hana mwanzo wake Wala mwisho wake na hangehitaji kuumbwa ili awepo wala hategemei chochote ili aendelee kuwepo, wala hakuna mazingira yoyote yanaweza kusababisha asiwepo.
Kwa vile Mungu ni Roho, basi yeye hufikiri kwa kiwango kisicho na mipaka ya utambuzi. Kwa sababu roho, super conscious mind ni ufahamu usio na mipaka katika utendaji na utambuzi. Kwa kuwa Mungu ni Roho basi Mungu ni ufahamu usio na mipaka katika utendaji na utambuzi. Mungu ni Roho na ni chanzo cha nguvu zote.

UKAMILIFU WA KAZI YA MUNGU

Mungu ni mkamilifu. Kwa hiyo kazi yake sharti iwe kamilifu. Kazi yote ya Mungu ni kamilifu katika nyanja zake zote. Kila kitu alichofanya tazama ni chema sana. Ulimwengu wote umekamilika katika uumbaji wake, unajitosheleza na kujitegemea wenyewe. Hauhitaji Mungu aje kurekebisha chochote, maana kufanya hivyo kungeonesha kwamba kazi yake si kamilifu. Lakini sasa kazi yake ni kamilifu na kwa hiyo ulimwengu wote ni mkamilifu. Hata wanadamu ni wakamilifu kabisa.
Sehemu za Ukamilifu wa kazi ya Mungu
Ukamilifu wa kazi ya Mungu umegawika katika sehemu mbili.
Sehemu ya kwanza :Ukamilifu unaotenda kazi (Dynamic perfection)
Huu ni Ukamilifu ulioanza kutenda kazi kikamilifu tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu. Ukamilifu huu unatenda kazi kupitia Kanuni za Asili. Ukamilifu huu ni kama robo tatu hivi katika mazingira ya binadamu.

Sehemu ya pili: Ukamilifu tuli (Static perfection)
Huu ni Ukamilifu uliomo ndani ya Mamlaka ya Nafsi. Wenyewe hautendi kazi hadi uruhusiwe na binadamu. Ukamilifu huu ni kama robo tu ya Ukamilifu wote wa kazi ya Mungu. Ukamilifu huu tuli, unavumbuliwa taratibu kupitia wanadamu ili kukamilisha 100% ya Ukamilifu wa Kazi ya Mungu.


NGUZO ZA JUMUIA YA UNYOFU

itaendelea muda si mrefu.............



No comments:

Post a Comment