UWEZO USIO NA MIPAKA WA BINADAMU

Uwezo usio na mipaka wa binadamu. 

Wakati dini zingine zikimfafanua binadamu kama kiumbe dhaifu asiyejiweza katika lolote, Unyofu unafundisha kwamba binadamu anaweza yote, hii ni kwa sababu ya uungu wa Mungu mwenyewe uliomo ndani yake. Miongoni mwa sifa asili aliyoumbwa nayo mwanadamu ni akili ya Mungu mwenyewe ndani yake, sehemu hii ya tatu ya ufahamu wa mwanadamu inayojulikana kwa wengi kama roho ama super conscious mind ni sehemu ya Mungu mwenyewe ndani yetu, ni Uungu wenyewe wa Mungu ndani yetu, sehemu hii kwa sababu ni uungu wenyewe inaweza yote, inafahamu yote, Ina majibu yote, na bado sehemu hii ni mtumishi wetu, tunaruhusiwa kuitumia muda wowote, katika jukumu lolote na kwa sababu hiyo binadamu hana mipaka katika uwezo wake katika sayansi ya kiroho ama sayansi ya Asili.
Sayansi ya kiroho, hii inayoitwa utendaji wa miujiza, n.k , au sayansi ya Asili kama bayolojia, kemia, Fizikia n.k, vyote havina mwisho katika ukuaji wake.


Unyofu unaamini kwamba ukuaji wa maarifa ya binadamu ndio msaada pekee wa binadamu, binadamu hana uwezekano mwingine wa kuondoa matatizo yote yanayomkabili zaidi ya ukuaji wa maarifa. Historia yote ya jamii ya binadamu ndivyo inavyozungumza kwamba binadamu tangu kuwapo kwake ameweza kuondoa tangu tatizo dogo kabisa, hadi tatizo kubwa na bado teknolojia yaendelea kuongezeka na kuondoa cha za binadamu moja baada ya nyingine. Ukuaji wa maarifa unaendelea kuongezeka na changamoto duniani zinapungua moja baada ya nyingine. Tangu kuvumbuliwa kwa moto, nguo, umeme, usafiri, mawasiliano, viwanda, n.k

Sisi Wanyofu kwa sababu hiyo hatungojei kiumbe yeyote kuja kutatua matatizo yetu. Matatizo yote yana majawabu katika ukuaji wa maarifa. Mungu hutumia watu kutatua matatizo ya watu
Sote tunatambua kwamba hapo awali binadamu amekuwa akiishi tu porini uchi, bila moto, bila nyumba wala shamba, lakini binadamu huyo bado alikuwa tofauti na wanyama wenzake wa porini kwa sababu yeye alikuwa na uwezo wa kuongezeka kwa maarifa na taratibu maisha yake ya kaanza kuwa tofauti na wanyama wengine. Uduni mmoja baada ya mwingine umekuwa ukiangushwa njiani kwa kadiri Jamii binadamu ilivyokuwa ikisonga mbele, hadi hivi leo tunaitwa Jamii yenye teknolojia lakini kumbe mambo bado maana ni asili 10 tu ya akili iliyotumika hadi sasa. Itakapofikiwa 90 % ya akili ya binadamu, matatizo yote yatakuwa yameondolewa duniani, na teknolojia yote ya uhai kuanzia unavyotengenezwa hadi unavyozuiwa usidhurike hadi unavyorudishwa kwa upya, teknolojia hiyo itakuwa ni miongoni mwa teknolojia za kawaida tu duniani.

  (BOFYA HAPA kusoma Uelewa mzima UNYOOFU UNAAMINI NINI?).

No comments:

Post a Comment