KWA NINI TUNAITWA WANYOFU

KWA NINI TUNAITWA WANYOFU?

Unyofu ndilo jina mama la dini. Karibia dini kuu zote zilizopo leo ni matokeo ya dini mbili za zamani sana. Dini hizo mbili ni Judaism na Hinduism.
Sasa jambo la msingi linalopaswa kufahamika hapa ni kwamba waasisi wa dini hizi mbili hawakuwa wakiitwa Wayahudi wala Wahindu.
Waasisi wa dini ya Kihindu waliwasili ktk bonde la mto Ganges takribani miaka 3500 iliyopita. Watu hawa walijulikana kama "Aryan" Chasema kitabu, jitihada za aina binadamu kumtafuta Mungu . 

Aryan ni neno la kiajemi, maana yake "Wanyofu"
Waasisi wa dini ya Kiyahudi, walijulikana kama "Yeshurun" jina la lugha ya kiebrania, lenye maana ya "Wanyofu" kwa Kiswahili.
Ktk maandiko ya kiebrania utakutana na neno Yeshurun, mara kadhaa - Kumb, 32 :15,33:5,26. Na katika Isaya 44:2.
Sasa Jina Yeshurun, halikuwa jina la ukoo, kwa vile hakuna miongoni mwa wazee wao kama Ibrahim, Isaka au Yakobo aliyejulikana kwa jina hilo.
Chasema kitabu cha SDA BD , article Jeshurun, "Jina hilo ni jina lenye kuonesha aina ya mwenendo Mungu aliokusudia wafuate" Kwa maana maagizo yote waliyopewa kutoka kwa Mungu, yaliweza kutafsiriwa kwa neno moja tu - Unyofu. Kwa kifupi Mungu alikuwa akiwaambia - "Iweni Wanyofu.
Dhana hii inaungwa mkono pia na maandiko hayo ya kale ambapo yanathibitisha kwamba" Mungu alimfanya mwanadamu Mnyofu, lakini wamebuni mavumbuzi mengi "-Mhubiri 7:29, na kwamba " Njia (dini) ya mwenye haki ni Unyofu - Isaya 26 :7,8.
Hivyo basi kwa mujibu wa maandiko hayo na mengineyo mengi, sisi Wanyofu tunaamini kwamba wanadini hao wa kale watu kama Ibrahim, Nuhu, Ayubu,Musa au Yesu, walikuwa ni Wanyofu wenzetu maadamu walikuwa wenye haki kwa maana - Njia (dini) ya mwenye haki ni Unyofu.

No comments:

Post a Comment