Wanyofu hatuamini uwepo wa kiumbe cha kusadikika, shetani. Sababu
zote zote zitolewazo kuthibitisha uwepo wa kiumbe huyo wa uongo
hazikidhi viwango, kwa sababu kimsingi binadamu ni mwenye uwezo wa
kuchagua mema au mabaya kwa hiyo si lazima awepo kiumbe mwingine
kumkatisha shauri katika chaguzi zake hizo. Binadamu yeye binafsi ana uwezo
wa kuchagua mabaya na yeye huyo huyo anao uwezo pia wa kuchagua mema.
Aidha pia matatizo mbali mbali yaliyopo ulimwenguni sio matokeo ya uwepo
wa shetani, mfano malaria sio matokeo ya shetani, ni matokeo ya
plasmodium, ukiugua Malaria maana yake umeng'atwa na mbu waenezao
malaria na shetani kwa vyo vyote hajahusika hapo. Kwa kifupi Wanyofu
tunasema uwepo wa matatizo duniani ni matokeo ya uchanga wa Mamlaka ya
Nafsi, pamoja na matumizi mabaya ya Mamlaka ya Nafsi.
Uwepo wa
kiumbe huyo wa uongo mioyoni mwa watu kumepelekea changamoto nyingine
kuongezeka duniani, kwa sababu dini zimekuwa badala ya kuleta amani
duniani zimechangia umwagaji damu wa kutisha zaidi kwa sababu kila dini
ilimhisi shetani nyuma ya dini nyingine, wakatoliki barani Ulaya wameua
mamilioni ya wakristo wacha Mungu kisa tu kanisa liliwaona wazushi yaani
wamefuata mafundisho ya shetani , waislamu katika vita zao za jihad, hadi
leo matukio ya kujitoa mhanga dini zinahisi zinamtumikia Mungu kwa
kuangamiza wafuasi wa shetani.
Watu
badala ya kukaa chini na kutafuta suluhu za kudumu kwa changamoto zao
za kiroho, kiakili, kimwili na kiuchumi, ndoa nyingi zinaparanganyika
lakini jawabu linakuwa jepesi tu siku zote , dini zinatoa jibu jepesi tu
kwamba dunia haitawezekana kutengemaa
kwa sababu humu duniani kuna shetani, ambaye anaonwa kuwa na Nguvu
kuliko binadamu na kwa hiyo hamna jinsi, hamna Tumaini tena humu
duniani. Jitihada zo zote zinaazofanywa na binadamu kujikomboa na
umaskini na majanga mbali mbali zinaonekana kama tu kichekesho kwa dini
za kale.
(Kwa Maelezo mengineyo ya ziada BOFYA HAPA)
Kwa
vyo vyote uwepo wa shetani ni simango kwa Mungu na ni kama kuonesha
kwamba hajui kupangilia na kwamba anazidiwa hekima na sisi viumbe wake,
maana awezaje kumtupa humu duniani kama vitabu vinavyosema au hata
kumruhusu kiumbe wa hatari, mwenye nguvu kuliko
sisi kumruhusu aje humu baada ya kushindikana mbinguni? Kisha sababu
ya udhaifu wetu mbele ya kiumbe huyo ikabidi tuanguke licha ya kutopenda
kufanya hivyo, lakini tena Mungu huyo huyo aamue kutuchoma moto usio na
mwisho, milele na milele na milele, na milele na milele, na
milele--Mungu mwenye maamuzi ya hivyo kwa vyo vyote hana
upendo wala hekima wala uadilifu.
(BOFYA HAPA kusoma zaidi KUHUSU WANYOFU).
No comments:
Post a Comment